24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waliopona Corona Afrika ni zaidi ya 3,000

ADDIS ABABA, ETHIOPIA

TAKWIMU mpya za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonyesha kuwa, watu 3,235 waliokuwa wameambukizwa virusi vya corona katika nchi 52 za Afrika wamepata afueni.

Takwimu hizo zilizotolewa mapema jana (Aprili 15) zinasema kuwa, kesi 16,265 za wagonjwa wa Covid-19 zimethibitishwa kufikia sasa katika nchi hizo za Afrika.

Kwa mujibu wa  Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, watu 873 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona barani Afrika.

Nchi 52 za Afrika zimeathiriwa na virusi vya corona huku nchi mbili za Lesotho na Comoro zikiwa hazina kesi yoyote hadi sasa ya ugonjwa huo angamizi wa kuambukiza.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Algeria inaongoza kwa idadi ya vifo na maambukizo barani Afrika na kwamba hadi sasa, watu zaidi ya 300 wamekufa kwa corona katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika na walioambukizwa ni karibu 2,000.

Marekani inaongoza kwa maambukizo na vifo vya corona duniani, ambapo hadi jana mchana watu 2,228 waliaga dunia na kusababisha idadi ya walipoteza maisha kwa ugonjwa huo hadi sasa katika nchi hiyo kufikia 28,300.

Waliokufa kwa Corona kote duniani hadi sasa ni zaidi ya 120,000 huku idadi ya walioambukizwa virusi hivyo ikikaribia milioni 2.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles