23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Askari polisi, magaidi saba wauawa

CAIRO, MISRI

OFISA wa Polisi wa Misri na washukiwa saba wa genge la kigaidi wameuawa katika makabiliano ya risasi baina ya pande mbili hizo jijini Cairo.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ilisema jana kuwa makabiliano hayo yalitokea juzi Jumanne katika Wilaya ya al-Amiyira, viungani mwa mji mkuu, Cairo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, askari polisi wengine watatu walijeruhiwa katika mapambano hayo ya risasi, lakini maofisa usalama walifanikiwa kuwaangamiza magaidi saba, mbali na kutwaa silaha zilizokuwa zinatumiwa nao.

Wiki iliyopita pia, jeshi la Misri lilizishambulia ngome za magaidi katika eneo la Sinai Kaskazini mwa nchi hiyo kufuatia kuongezeka mashambulizi ya magaidi. 

Operesheni hiyo ya maofisa usalama ilijiri siku chache baada ya magaidi kufanya mashambulizi pambizoni mwa eneo la Rafah na kumuua mwanajeshi mmoja wa Misri na kuwajeruhi wawili. 

Makundi ya kigaidi huko Misri yameelekeza hujuma na mashambulizi yake katika Mkoa wa Sinai ya Kaskazini na wakati huo huo pia yanafanya hujuma katika maeneo ya katikati na Kusini mwa Sinai na vile vile katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Kundi liitwalo Ansarul Baitul Maqdis ambalo limebadili jina lake na kuwa kundi la Mamlaka ya Sinai baada ya kuungana na kundi la kigaidi la Daesh, ndilo linalotekeleza mashambulizi mengi dhidi ya askari wa Misri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles