25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wakuu wa mikoa, wilaya kuanza mafunzo ya uongozi wiki ijayo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imesema viongozi wa umma walioteuliwa katika nyadhifa mbalimbali pamoja na wale ambao wamepata nafasi hizo kutokana na sifa zao wanatarajiwa kuanza mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi ambapo kwakuanzia wiki ijayo wataanza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Waziri wa Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mohammed Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 18, 2021 alipokuwa akizindua Bodi ya tatu ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uongozi ambayo imeteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassa ambapo Mwenyekiti wake ni Dk. Stergomena Tax.

Amesema mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kutolewa kwa viongozi wote kama ilivyoelekezwa hivi karibuni na Rais Samia yana lengo la kuwajengea uwezo wakimaadili viongozi wa umma nchini.

“Lengo letu ni kuhakikisha viongozi wa umma wanapata mafunzo haya ili waweze kujengeka kimaadili,viongozi waweze kujua mipaka yao katika katika jamii na pia atambue kuwa uongozi ni koti,”amesema Mchengerwa.

Amefafanua zaidi kuwa serikali haitegemei baada ya mafunzo hayo kuona kiongozi anaenda kinyume na maadili na kufanya kazi bila kufuata haki na miongozo.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali itaendelea kukiangalia chuo cha taasisi ya uongozi kwa karibu ili kuhakikisha kinarejea katika sifa yake ya kuwa chuo cha viongozi.

Kwa upande wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya Uongozi, Dk.Stergomena amesema kuwa taasisi hiyo inaelewa dhumuni la kujenga na kuandaa viongozi ambao wataleta maendeleo endelevu katika nchi ni wajibu wao kuhakikisha wanafanya hivyo.

“Kutoa mafunzo haina maana kwamba Tanzania hakuna viongozi lakini elimu haiishi, tunawapa mafunzo kwa lengo la kuleta maendeleo, taasisi inatambua umuhimu wa kuwa na viongozi mahili watakaochangia kuendeleza nchi,”amesema Dk.Stergomena.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo alisema taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo kwa viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ili kuweza kuwasaidia viongozi wa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles