22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Simba yataja siku ya kutangaza ubingwa

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema wakishinda michezo mitatu ijayo wanatangaza ubingwa. Simba kesho inashuka dimbani kuikabili Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maandalizi ya mchezo huo, Matola amesema wachezaji wake wapo tayari kupigania pointi tatu.

Amesema Polisi Tanzania haijawahi kuwafinga katika michezo yote mitatu waliyokutana, miwili msimu uliopita na mmoja msimu huu.

“Tumewafunga katika mechi zote tatu za ligi tulizokutana nao, lakini haimaanishi mechi ya kesho itakuwa rahisi kwetu, tutaingia kwa tahadhari na lengo letu ni kushinda ili kusogelea ubingwa wa ligi,” amesema Matola.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema morali za wachezaji ipo juu na kilicho vichwani mwao ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo ili kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles