23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Zambia yatangaza siku 21 za kuomboleza kifo cha Kaunda

Lusaka, Zambia

Serikali ya Zambia imetangaza kipindi cha siku 21 kufuatia maombolezo ya kitaifa ya kifo cha Rais wa kwanza wa Taifa hilo Kenneth Kaunda.

Kaunda alifariki jana jioni Juni 17, 2021 katika hospitali ya jeshi mjini Lusaka akiwa na umri wa miaka 97.

Kupitia moja ya Mtandao wa kijamii wa Rais wa sasa wa Zambia Edgar Lungu amesema hayati Kaunda alikuwa shujaa wa kweli wa kiafrika.

Pia waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Zambia kupitia ukurasa wake wa Ukurasa wake wa kijamii ameandikakuwa amesikitishwa na kifo cha Kaunda.

Kaunda alipigania ukombozi wa nchi yake kutoka ukoloni wa Waingereza hadi uhuru ulipopatikana mwaka 1964 na kuwa rais wa kwanza wa Zambia huru.

Wakati wa utawala wake wa miaka 27 alisifika kwa kupendelea njia za amani kutatua mizozo na kusaidia harakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles