23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WATAKA BODI YA PAMBA IVUNJWE

Na SAMWEL MWANGA


WAKULIMA wa  pamba   mkoani Simiyu wameitaka serikali kuivunja Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kwa kuwa imekuwa na kiburi.

Wamedai bodi hiyo inataka kuua biashara ya bei ya zao hilo huku wakulima wakinyanyasika.

Vilvile  wamewataka viongozi   serikalini wanaoikumbatia bodi hiyo kuacha mara moja kwa kuwa  imekuwa hata ikishindwa kutekeleza maagizo mbalimbali  yanayofikiwa na mkutano mkuu wa wadau wa zao hilo ikiwamo   kuwapo   mashamba ya kuzalisha mbegu za   pamba.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi, walisema   wanashangazwa na kitendo cha bodi hiyo kugeuka kuwa  ndiyo msimamizi mkuu wa upangaji wa bei ya pamba   kwa mkulima wa pamba badala ya kusaidia kilimo hicho kikue.

Walisema    umefika wakati kwa bodi hiyo kuvunjwa kwa sababu imeshindwa kuendeleza zao hilo na kila kukicha mkulima wa   pamba amekuwa akinyanyasika huku watumishi wa bodi hiyo wakiendelea kuneemeka kupitia jasho la wakulima.

“Mimi nataka serikali kupitia  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi avunje bodi hii kwa sababu kazi yake ni kupanga bei ya pamba badala ya kuwasaidia wakulima kuendeleza kilimo hicho “Hata bei wanayopanga ni ya kumnyanyasa mkulima huku wao wakiendelea kunufaika kwa kutumia jasho letu sisi wakulima,” alisema Khija Malimi.

Madirisha Saguda alisema watu milioni 16   wanategemea kilimo hicho na wamekuwa wakilia kila siku kupata soko zuri la zao hilo lakini bodi hiyo imekuwa haina faida kwao.

Alisema  hivyo ivunjwe na kusisitiza kuwa  ndiyo mchawi mkubwa wa zao hilo hivyo haina umuhimu ivunjwe tu.

“Wakulima tupatao milioni 16   nchini tunaolima zao hili la pamba kila mwaka tumekuwa tukililia tupate bei nzuri ya pamba kutokana na gharama kuwa kubwa za uzalishaji.

“Lakini kinachotokea ni hawa bodi ya pamba wanakuja na kutupangia bei  kwa maslahi yao na kwa uhalisia mchawi wa   pamba ni bodi yetu hii ya pamba, naona haina umuhimu ni vizuri ikavunjwa,”alisema Saguda.

Naye Mayunga Kisena alisema bodi hiyo imekuwa ni kikwazo cha kuendeleza zao hilo kwa vile  imekuwa ikimkandamiza mkulima  na wafanyabiashara wadogo  wa zao hilo huku w wafanyabiashara wakubwa wakikumbatiwa kwa manufaa yao binafsi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga,   alisema  bodi hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa ujanjaujanja.

Alisema bodi hiyo inashindwa hata kusimamia maagizo yaliyopitishwa kwenye mkutano wa mwaka jana wa wadau wa zao hilo ya kutaka   ianzishe mashamba ya kuzalisha mbegu ya zao hilo,   badala yake inatumia mashamba ya wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles