29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

HALOTEL YAFAFANUA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu  baadhi ya makosa yaliyohusishwa na kampuni hiyo pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo, ikisema kuhusishwa kwake kunatokana na vipengele viwili.

Mashtaka hayo ni kushindwa kutoa taarifa za usajiri wa kampuni ya UNEX Company Ltd kwa ajili ya kusajili laini za simu 1000 zilizouzwa kwa kampuni hiyo pamoja na kutotimiza majukumu yake vizuri kwa kuuza laini za simu 1000 kwa Kampuni ya UNEX ambayo haijasajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kutokana na makosa hayo mahakama iliitia hatiani kwa kuisababishia Serikali hasara ta Sh milioni 459 kwa kufanya mawasiliano nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai, alizungumzia katika hati ya mashitaka iliyosainiwa na mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali Mei 16,  mwaka huu.

Alisema  makosa hayo  mawili,   hasa namba  sita na saba,   hayahusiani kampuni hiyo   kwa vile  washtakiwa wengine ambao ni raia wa Pakistan si wafanyakazi wa kampuni hiyo na   hawana ushirikiano wowote na kampuni hiyo.  

“Tulipohusika na kuhusishwa kwao ni kosa letu la kuwauzia laini za simu ambazo hazijasajiliwa na kutowasilisha nyaraka zisizo halali.

“Sisi ni kampuni inayofanya kazi kwa usajiri na vibali halali tulivyopewa na mamlaka ya nchi hii na tumekuwa wawazi na kufuata taratibu na sheria.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles