24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WA MBOGA WAONDOLEWA IGOME

Na TIGANYA VINCENT-TABORA


KAMATI ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Tabora imeendesha operesheni ya kung’oa mazao mbalimbali ya bustani yaliyokuwa yamepandwa na wavamizi katika maeneo ya vyanzo vya maji na kando mwa Bwawa la Igome na hivyo kusababisha uzalishaji wa maji kupungua.

Akiongoza operesheni hiyo jana, Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi, alisema wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kubainika kuwapo kundi kubwa la watu wanaoendesha kilimo cha mazao mbalimbali, ikiwamo matunda na kuhatarisha afya za watumiaji.

Katika operesheni hiyo, mazao mbalimbali kama vile majani ya maboga, hoho, nyanya na matembele yaling’olewa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo, Mlozi alisema wavamizi hao wamekuwa wakiendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo vya bwawa hilo, ikiwamo kilimo cha mbogamboga na wamekuwa wakiweka dawa ambazo wakati mwingine zimekuwa zikiingia katika maji hayo, ambayo wakazi wengi wa Wilaya ya Tabora wanayatumia.

DC Mlozi alisema maji hayo yasipowekewa dawa vizuri ya kusafisha upo uwezekano wa watumiaji kunywa dawa za kilimo zilizotoririkia majini.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Tabora (TUWASA),  Christopher Shinyanza, alisema wavamizi hao wamesababishia kina cha maji kupungua na kusababisha gharama za uzalishaji ili yamfikie mtumiaji yakiwa safi bila kuwa na tope litokanalo na kilimo kando kando ya bwawa hilo.

“Shughuli za kilimo katika vyanzo vya maji vya bwawa hili zimesababisha kupungua uzalishaji wa maji kwa ajili ya matumizi  kwa wakazi wa Manispaa ya Tabora, hasa kipindi hiki cha kiangazi, ukilinganisha na kipindi cha masika,” alisema.

 

Shanyanzi alisema wakati wa masika kwa sababu ya kupata mvua waliweza kuzalisha wastani wa mita za ujazo 16,500, ambazo kwa kiasi kikubwa  yalikuwa yakitosha, lakini kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kilimo katika bwawa hilo, hivi sasa wanazalisha mita za ujazo 11,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles