WOLPER: CHEREHANI INALIPA ZAIDI YA FILAMU

0
1555

Na KYALAA SEHEYE


STAA wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper, ameibuka na kudai kwamba ufundi cherehani ndiyo unaomlipa zaidi kuliko filamu alizowahi kucheza.

Kutokana na kauli hiyo, mwigizaji huyo ambaye kwa sasa ni mjasiriamali anayekua kwa kasi, ameweka wazi mpango wake wa kuanza kuwashonea nguo watu maarufu ndani na nje ya Tanzania ili aingie kwa nguvu kwenye orodha ya wabunifu wenye majina makubwa duniani kote.

Licha ya madai hayo, Wolper alisema anaiheshimu sanaa kwa kuwa ndiyo iliyomtambulisha kwa jamii na kumwezesha kufanya shughuli zake nyingine kwa urahisi, lakini baada ya kuingia katika ushonaji wa nguo za mitindo mbalimbali, anaona inalipa zaidi ya filamu.

“Sikuwahi  kufikiria kama ufundi cherahani unaweza kuwa na pesa hasa ukiwa mbunifu mzuri wa mitindo ya nguo, kwa sasa nategemea zaidi kazi hii kuliko uigizaji na kutokana na hilo nitafanya filamu chache tu kwa mwaka ili akili yangu kubwa nielekeze kwenye biashara ya ushonaji,” alisema Wolper.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here