29.7 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima 949,643 wanufaika na mbolea ya ruzuku nchini

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Wakulima 949,643 wamenufaika na mbolea ya ruzuku hadi kufikia Juni, mwaka huu kati ya milioni 3.3 waliosaijiwa tangu utaratibu huo uanze Agosti, mwaka jana.

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Julai 17,2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dk. Stephen Ngailo wakati taarifa ya utekelezaji na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2023/24.

Hata hivyo, amesema lengo la kuwasajili halikuwa kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku pekee bali kupata huduma nyingine ikiwemo za ugani na pembejeo.

“Kiasi cha mbolea ya ruzuku kilichonunuliwa kwa ruzuku ni tani 383,219 hadi kufikia Juni mwaka huu,”amesema.

Kwa mujibu wa takwimu za mamlaka hiyo, Mkoa wa Mtwara unaongoza kwa ununuzi wa mbolea hiyo baada ya kununua tani 332,602, Ruvuma (323,947) na Simiyu (220,094).

Kwa upande wa mikoa iliyonua kidogo na tani walizonunua katika mabano ni Dar es Salaam (5431), Mara (40,267) na Shinyanga (58,003).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles