23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

PPRA yazibana kampuni zilizokiuka sheria

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imezifungia baadhi ya kampuni kwa kukiuka sheria na kwenda kinyume na utaratibu wa sheria za ununuzi wa Umma ikiwa ni pamoja kufanya udanganyifu wa kughushi nyaraka za taarifa za fedha za benki.

Hayo yameelezwa leo Julai 17,2023 jijini hapa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Eliakim Maswi, wakati akieleza utekelezaji na mwelekeo wa majukumu ya Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mtendaji huyo amesema wamezifungia kampuni kadhaa kufuatia makosa mbalimbali ikiwemo ya udanganyifu wa kugushi nyaraka za taarifa za fedha za benki, na taarifa za malipo ya awali ya benki.

Maswi amesema mikakati iliyopo kwa Mamlaka hiyo kwa sasa ni kuboresha tatizo la ununuuzi wa Umma liwe ni suala la uwazi ili kusiwe na mianya ya rushwa.

Amesema ukosefu wa uwazi katika mchakato wa ununuuzi wa Umma kunasababisha changamoto za upatikanaji wa taarifa za zabuni, thamani ya mkataba na kusababisha ukosefu na uaminifu na imani kwa Taasisi za Umma.

Maswi amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilion 40 kwa PPRA ili iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwemo na kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka hiyo.

“Serikali imekuja na Mfuko mpya wa ununuuzi wa Umma kwa njia ya kielektroniki (NeST) kufuatia Serikali kutumia fedha nyingi zinazoidhinishwa kwenye bajeti kwaajili ya ununuuzi wa bidhaa, kandarasi za ujenzi na huduma kuzingatia matakwa ya Sheria ya ununuuzi wa Umma sura 410,”amesema Mtendaji huyo.

Aidha Mtendaji huyo amesema moduli ya kusimamia mikataba iliyomo katika mfumo mpya wa manunuzi wa NeST itakamilika mwishoni mwa mwaka 2023.

“Moduli ya kusimamia mikataba inataka lazima mikataba yote (ya manunuzi) tunayoifanya ionekane katika mfumo ili hata ukifanya mabadiliko ya vitu na bei ionekane katika mfumo. Tunategemea ikamilike kabla ya mwisho wa mwaka huu,”amesema.

Amesema lengo la kujenga mfumo huo wenye moduli sita, ni kuongeza uwazi kwenye ununuzi wa umma, usizi mzuri wa fedha za uma, kudhibiti vitendo vya rushwa na ufuatiliaji wa ukidhi wa sheria na uwajibikaji wa ununuzi,”amesema na kuongeza kuwa:
“Katika mfumo huo mpya ambao moduli zake mbili zimekamilika zimeanza kutumiwa na tangu Julai Mosi mwaka huu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles