22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi wa kitongoji cha Boza, Makurunge wamlilia Rais Samia

Na Esther Mnyika, Bagamoyo

Zaidi ya wananchi 5,826 wa Kitongoji cha Bozi Kata ya Makurunge wamemuomba Rais, Dk. Samia Suluhu kama kuna mradi wowote unatarajia kuanza katika maeneo hayo watengewe makazi ya kudumu yenye huduma za kijamii.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wakazi wa Kitongoji cha Bozi Kata ya Makurunge, Nawahi Vicent Nawahi.

Wananchi hao wamepaza kilio hicho Agostii 19, wilayani Bagamoyo katika mkutano wa hadhara ambao pia ulihusisha Waandishi wa Habari ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Wananchi wa Kitongoji cha Boza, Nawahi Nawahi alisema wao hawana uongozi wa Serikali wowote kitongoji kilivunjwa tangu mwaka 2019 wanajiendesha wenyewe hadi sasa.

Amesma Kitongoji hicho kilivunjwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Majid Mwanga hakutoa sababu ya kuvunja Kitongoji hivyo hawana shule, zahanati na huduma nyingine za kijamii.

“Tunamuomba Rais Dk. Samia atusaidie hatakama kuna mradi wowote watutengee makazi yetu sisi ni wa kazi wa hapa bozi na ni wapigakura wake na sio wavamizi tumeishi kwa mda mrefu tuna familia zetu shughuli za kijamii zinaendelea,” amesema Nawahi.

Ameeleza kuwa eneo hilo lina mzunguko wa hekta 28, mwaka 1985 ambapo Rais wa awamu ya kwanza Hayati Baba wa Taifa, Julias Nyerere aligawa hekta 6,000 kwa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya lanchi ya mifugo ambapo kampuni ya Lazaba ilishindwa kuendeleza lanchi hiyo watu wakaanza kuishi.

Nawahi amesema walipata mshtuko baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abukar Kunenge Juni 6, mwaka huu kutoa tamko akiwataka waondoke kwa kuwa ni wavamizi katika eneo hilo.

Naye Mkazi wa eneo hilo, Furaha Mwakajuma amesema wanaomba Rais Dk. Samia Suluhu kuingilia kati jambo hilo kwani wao ni Watanzania na wamekuwa hapo kwa miaka 40 sasa.

“Eneo hili lina mzunguko wa hekta 28 limegawanya sehemu tatu hekta 6,000 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hekta 10 za Bakharesa hekta 12 na Wakala wa Misitu (TFS) tumeambiwa tuondoke twende wapi? maisha magumu sana kuanza maisha tena sehemu nyingine tuna familia umri umeenda,” amesema Mwakajuma.

Naye, Mkazi wa eneo hilo, Mzee Hussen Abdalah amesema tangu mwaka 1938 yupo Kitongoji hicho kwa sasa anatimiza miaka 86 wanasema aondoke ataenda wapi? Wao sio wavamizi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Mkazi wa eneo hilo, Evelina Jeremia amesema tangu kufutwa kwa kitongoji hicho hadi sasa hawajui sababu wamekuwa wakiendeleza shughuli zao wenyewe hawana hata mwenyekiti wa mtaa.

“Sisi tunaomba serikali itupatie ardhi sehemu ambayo tunastahili tuendelee kwa sababu hadi sasa kuna shughuli mbalimbali za kijamii zinaendelea Bozi na watusogezee huduma kwa sasa ili upate huduma kama watoto kwenda shule ilipo ni umbali wa kilomita 8,” amesema Evelina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles