24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkumbo atembelea banda la WHI Arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo leo Agosti 20, 2023 ametembelea banda la Watumishi Housing Investments (WHI) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) jijini Arusha ambapo Kikao Kazi cha Wakuu wa Taasisi za Umma na Wenyeviti wa Bodi kinaendelea.

Pamoja na mambo menjine Prof. Mkumbo amevutiwa na huduma zinazotolewa na Watumishi Housing Investments na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kuwahudumia Watanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa WHI, Dk. Fred Msemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya WHI CPA. Hosea Kashimba ni sehemu ya wanaoshiriki Mkutano huo uliofunguliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan Agosti 19, mwaka huu.

Kikao Kazi hicho kinahusisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma.

Watumishi Housing Investments (WHI) ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2014 chini ya sheria ya Makampuni (Cap 212) kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma na wanachama wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni matarajio katika malengo ya kitaifa na kimataifa kama yalivyoainishwa katika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi (2000), Dira ya Maendeleo ya 2025, na Malengo ya Maendeleo Endelevu: 2030.

Aidha, WHI inasimamia Mifuko ya Uwekezaji ambayo ni: Mfuko wa Uwekezaji katika Milki (REIT) na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (CIS) ambapo kwa sasa WHI inaendesha MFUKO WA FAIDA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles