21.4 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Hemant Punjabi awika Shining Star Africa Awards

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwanamuziki mwenye asili ya India anayeishi nchini Benin, amefanikiwa kuingia kwenyr tuzo kubwa barani Afrika za The Shining Star Africa Awards zitakazofanyika mapema mwezi ujao Afrika Kusini.

Punjabi anayetamba na wimbo Rock Your Body, amekuwa na ukaribu mkubwa na mastaa wa Afrika Mashariki kama vile Awilo Longomba na wengineo aliofanya nao kazi kwenye albamu yake ijayo.

Akizungumzia tuzo hizo Punjabi, amesema The Shining Star Africa Awards ni tukio adhimu la kusherehekea mafanikio bora katika nyanja mbalimbali za sanaa ndani ya Afrika na litafanyika jijini Johannesburg, frika Kusini likihudhuliwa na mastaa mbalimbali lengo likiwa ni kuonyesha utajiri wa vipaji vya kiafrika.

“Tuzo hizi zinaonyesha uwezo wa kujieleza kwa ki wasanii katika kuziba mapengo ya kitamaduni yaliyopo kwenye kizazi hiki na kukuza hali ya umoja miongoni mwetu, najisikia fahari kushiriki tuzo hizi, naamini ni muda mzuri kwangu wa kutangaza albamu yangu mpya ya From India To Africa (FITA),” amesema Punjabi ambaye ni balozi wa tuzo za Zikomo Awards, Zambia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles