30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wakali wa gofu kuchuana ‘ CRDB Inter Club Competition’

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Zaidi ya wachezaji wa gofu 120 kutoka klabu tatu tofauti wanatarajiwa kuchuana katika shindano ya mchezo huo ya ‘CRDB Inter Club Competition March 9,2024, kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Klabu hizo ni Dar es Salaam Gymkhana, Lugalo Gofu na Morogoro ambazo kila mmoja atatoa timu ya wachezaji 40 na wachezaji binafsi.

Akizungumzia shindano hilo mbele ya waandishi wa habari leo Februari 29,2024 jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari Klabu ya Lugalo, Meja Selemani Semunyu amesema lengo ni kujenga umoja na ushirikiano wa wachezaji kutoka katika klabu hizo.

Amewashukuru wadhamini ambao ni Benki ya CRDB kwa kuendelea kudhamini shindano hilo ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

” Kila klabu inajiandaa na iko tayari kushindana, kwa upande wetu Lugalo Golf Club tuko vizuri kuhakikisha tunaibuka washindi,” amesema Meja Semunyu.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa CRDB, Steven Adili amesema wanafamu umuhimu wa michezo ambayo ni ajira na itatoa fursa nyingi, hivyo kukutana kwa wachezaji hao watapata nafasi ya kubadilishana mawazi na kuleta tija kiuchumi.

“Tunajua michezo ni ajira, tutaendelea kushirikiana na Klabu ya Lugalo, pia tupo katika michezo mingine na tunaendelea hadi kwenye sarakasi tutaingia katika kwa sababu tunaamini ni chachu ya maendeleo,” amesema Adili.

Muwakilishi wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Ernest Sengeu amesema wachezaji hao watashiriki kwa kushindana pekee bali kudumisha umoja na kuendelea kukuza mchezo huo.

Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo, Meja Japhet Masai ametaja mfumo utakaotumiwa katika mashindano hayo ya siku moja kuwa ni “Match Play-Stroke Play Hole by Hole” yaani wachezaji wawili wa klabu moja watashindana nawawili wa klabu nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles