29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kujenga Chuo cha Ufundi Kata ya Liganga

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amesema Serikali imefanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu katika kipindi cha miaka mitatu.

Kauli hiyo ameitoa Wakati alipoongozana na Wenyeviti wa Mashina wa CCM katika kata ya Parangu, Mpandangido, Kilagano na Maposeni kujionea utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwenye ujenzi wa Miundo Mbinu ya Mambweni na Madarasa uliyofanyika katika shule ya sekondari Maposeni na Mtopesi Februari 28, 2024 katika Halmashauri ya Songea mkoani Ruvuma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) Peramiho, akiongozana na Wenyeviti wa Mashina wakikagua Mradi wa ujenzi wa Bweni katika shule ya sekondari Maposeni katika Halmashauri ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

Waziri Mhagama amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza, Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ili kupunguzia wananchi adhaa ya kuchangishana michango kwa ajili ya ujenzi. 

Katika shule ya Sekondari Maposeni kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 40, ambapo kuna madarasa ambayo ujenzi umekamilika na mengine yako mbioni kujengwa.

“Hivyo basi jamii inawajibu wa kumlinda mtoto wa kike na kumlinda mtoto wa kiume kwa kuwapatia elimu bora itakayosaidia kujenga Jamii yenye weledi,” amesema Waziri Mhagama.

Ameongeza kusema zawadi nyingine aliyotupatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha anafuta ada na kusaidia watoto wengi kwenda shule.

Kutokana na ongezeko la wanafunzi, tunahitaji kuongeza miundo mbinu ya elimu kwa ajili ya vijana wetu.

“Serikali inaandaa mitaala mpya ambayo itasaidia kuwapa elimu ya ufundi vijana wetu waweze kupata ujuzi,” amesema.

Sambamba na hilo, Halmashauri yetu ya Songea Vijijini, Serikali itajenga Chuo kikubwa cha Ufundi cha VETA katika Kata ya Liganga ili kuwezesha vijan kupata elimu ya ujuzi katika chuo hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Vijijini, Menace Komba amesema tayari wameshaanza utaratibu wa kuomba wizara ya elimu ili kupata kibali cha kubomoa majengo ya zamani ya shule ya sekondari Maposeni na Mpitimbi ili kujenga Madarasa mapya.

“Uamuzi huo umeafikiwa na Halmashauri ya Songea Vijijini ili kuipatia shule ya sekondari  Maposeni pamoja na Mpitimbi muonekano mzuri na wakuvutia,”alisema Komba.

Awali, Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mwalimu Dismass Nchimbi akizungumza mbele ya ujumbe wa wenyeviti wa Mashina alisema serikali imefanya mambo mengi katika shule ya sekondari Maposeni.

“Tumepata mradi wa ujenzi wa Mambweni 2, na Madarasa 4 na vyoo matundu 10 mradi unaofadhiliwa na Barick katika Jimbo la Peramiho,” alisema.

Serikali kupitia Mbunge wa Peramiho amesaidia pia ujenzi wa jengo jipya la utawala ambalo limegharimu kiasi cha Sh million 74 na ujenzi wake umefikia kwenye lenta

Akitoa neno la shukurani Mwanafunzi, Ahad Antony Bugari ameshukuru serikali kwa kuimarisha miundombinu ya elimu katika shule ya sekondari Maposeni.

Amemshukuru walimu wa Maposeni kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miundombinu ya elimu katika sekondari ya Maposeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles