24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Wajumbe wa mkutano mkuu CCM Ileje waridhishwa na utekelezaji wa Ilani

Na Denis Sinkonde, Songwe

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wameridhishwa na namna viongozi wa Halmsahuri ya Ileje wanavyotekeleza Ilani ya chama hicho ya mwaka 2020-2025 wilayani humo.

Wajumbe hao wamesema hayo wakati wa mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho wilayani humo ambao umefayika Februari 28, mwaka huu katika ukumbi wa CCM uliopo Itumba.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, wakiwa katika mkutano huo.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Hebron Kibona, pamoja na mambo mengine, mkutano huo umepokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzi mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2021 kutoka katika wilaya hiyo na baadhi ya taasisi ikiwepo TANESCO, TARURA, RUWASA na Idara ya Afya na Elimu.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba wilaya hiyo imepokea fedha mbalimbali za miradi ya maendeleo katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kufanikisha kuzisimamia kama ilivyoelekezwa.

Gidarya amesema katika sekta ya afya walipokea fedha za kukamilisha ujenzi wa maboma katika zahanati za vijiji vya Ilanga, Igoje na Chembe ambapo jumla ya Sh milioni 150  zilitolewa na kila zahanati kutengewa milioni 50 sambamba na fedha Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu za wagonjwa katika hospitali ya wilaya iliyopo Itumba.

Gidarya amesema pia serikali imetoa Sh milioni 250 zilizotokana na tozo ya miamala kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Ndola ambapo shughuli ya ujenzi inaendelea, pia zaidi ya Sh milioni 600 za Uviko-19 zilipelekwa katika halmashauri ya Ileje kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 30 vya  shule za msingi na sekondari.

Aidha, Gidarya imewapongeza mamlaka ya maji wilaya Ileje RUWASA chini ya usimamizi wa meneja wa mamlaka hiyo, Mhandisi Endrew Tesha, kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa baada ya tathimini kufanyika na kubaini wanaongoza kwa kila mwaka kuongeza vituo vya maji vijijini na kuzitaka idara zote kuiga utendaji na uwajibikaji kuzingatia Ilani ya CCM.

Mwenyekiti wa chama wilayani humo, Hebron Kibona fedha za miradi zinazopelekwa na serikali wilayani humo zinapaswa kusimamiwa ili wananchi waendelee kuneemeka na matunda na mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Katibu wa chama wilayani humo, Hassan Lyamba amesema katika kutekeleza mipango ya serikali ni wajibu wa wenyeviti na makatibu kata wa chama hicho kusimamia ajenda ya mapato ili kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.

Lyamba amesema usomaji wa taarifa hiyo kumeenda sambamba na uzinduzi wa ugawaji wa kadi za wananchama za kielektroni ambapo jumla ya wanachama 256 wanatarajia kugawiwa kwa awamu ya kwanza.

Katika kata ya Chitete wanachama 222, Ikinga 23, Bupigu 18, Itumba 2 na Mlale mmoja.

PICHA YA PILI WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM ILEJE.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles