28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Wajisaidia kwenye mabeseni kwa hofu ya kuuawa

beseniNa Ibrahim Yassin, Busokelo

WANANCHI wa Kata ya Luteba, Halmashauri ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wamebuni mtindo wa kujisaidia kwenye mabeseni usiku kwa hofu ya mauaji yanayodaiwa kuwa ya ushirikina.

Hatua ya wakazi hao ambao asilimia kubwa vyoo vyao viko nje, imekuja baada ya kuzuka kwa vitendo vya uporaji na mauaji ya kishirikina vinavyofanywa na baadhi ya watu baada kushauriwa na waganga kuwa watapata utajiri.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliotishwa ili kujadili hali hiyo, wananchi hao ambao wamekumbwa na taharuki, wamesema kuwa watu hao hushauriwa kufanya mauaji kisha wapeleke viungo vya binadamu watengenezewe dawa ya utajiri.

Walisema licha ya kujisaidia kwenye vyombo hivyo nyakati za usiku, imefikia hatua hata shamba hawaendi wakihofia kuuawa, na kwamba wakipeleka taarifa kwa viongozi wa Serikali za vijiji nao wanaogopa kuamka na kutoa msaada wakihofia kuuawa.

“Tumekuwa tukishuhudia mauaji ya utata, mara mtu kajinyonga, mara mtoto katumbukia shimoni kauawa na sasa wahalifu wameanza kukaba watu na kufanya uporaji.

“Tunaomba machifu na malifumu watupe maelezo kwanini wanashindwa kufanya ulinzi kwa wanakijiji ambao wamekuwa wakiuawa vifo vya utata,” alisema mmoja wa wakazi hao, Malisa Mwankemwa.

Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Furaha Mwasibata, alisema ni kweli malalamiko hayo yapo ingawa hana ushahidi wa jambo hilo.

“Kwa kuwa limezungumzwa kwenye mkutano wa hadhara, Serikali ya kata itachukua hatua ya kudhibiti hali hiyo, na kwa wale wanaojihusisha na vitendo hivyo nawaonya kuacha mara moja kabla hawajakutwa na mkono wa sheria,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles