25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wajawazito watahadharishwa dawa za kienyeji

BENJAMIN MASESE-MWANZA

SERIKALI imesema wanawake wa Kanda ya Ziwa wamekithiri kunywa dawa za kienyeji wanapokuwa wajawazito kwa kuzichanganya kwenye uji na chai kitendo kinachochangia vifo, kutokwa na damu nyingi  wanapojifungua, mimba kuharibika au kujifungua watoto wenye ulemavu.

Pia imetaja sababu kuu tatu zinazosababisha watoto wachanga  25 kati ya vizazi hai 1,000 kufariki  dunia ni kushindwa kupumua  ikiwa ni sawa na asilimia  31,  kuzaliwa chini ya uzito (njiti) asilimia 25 na maambukizo ya maradhi mbalimbali yakiwamo  Ukimwi  ikiwa ni asilimia 20.

Hayo yamebainishwa jana na Afisa Programu ya Uzazi Salama kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Martha Shakinyau  jijini Mwanza katika semina kwa waganga wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Shakinyau alisema amekuwa akizunguka katika hospitali mbalimbali nchini  kutoa elimu  ya uzazi salama kwa mama lakini amekutana na vituko vingi katika mikoa ya kanda hiyo.

“Ni jambo la kushangaza unakuta mama amekuja kwenye watalaam wa afya kujifungua lakini muda wote utaona ndugu zao wanampa dawa za kienyeji.

“Nyingine wanachanganya  kwenye uji na chai  sasa kitendo kile  ni hatari sana kwani madaktari wanakuwa wanatoa dawa za kitalaam huku kumbe mama kanyweshwa miti asili.

“Matokeo yake unakuta mjamzito anatokwa na damu nyingi na kufariki, mtoto naye akibahatika  kupona unakuta naye ana kasoro.

“Nimeshuhudia katika hospitali fulani nikiwa getini ndugu wa mjamzito wakilalamika wamepeleka chupa ya chai yenya dawa na uji ambao haukuwa na dawa, sasa wauguzi walimpa uji badala ya chai.

“Kumbe walitaka mjamzito anywe chai ambayo ina dawa asili ambazo wanaziamini angejifungua salama, nikafuatilia huyo mgonjwa  wodini nikakuta  ana hali mbaya na muda mfupi akawa amefariki,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles