22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mwanamama kortini kujeruhi kwa wembe

Mwanamama kortini kujeruhi kwa wembe

AVELINE KITOMARY Na                                            

COSTANCIA MUTAHABA (DSJ)

-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imempandisha kizimbani Asia Mohamed (26), mkazi wa Magomeni Mapipa kwa shtaka la kujeruhi.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Matarasa Hamisi, alidai kuwa Januari 5, mwaka huu eneo la Magomeni, Wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa alimkata kwa wembe sehemu za kidevu Idd Nasri, akimtuhumu kumchonganisha na mzazi mwenzake kitendo kilichosababisha kukosa matumizi ya mwanaye.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa mashtaka ukisema upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hata hivyo, Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaotoa bondi ya shilingi laki tano kwa kila mdhamini.

Mshtakiwa alikidhi vigezo vya dhamana na kuachiwa hadi kesi yake itakaposomwa tena Aprili, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, mahakama imempandisha kizimbani Salum Juma (24) mkazi wa Bunju A kwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Abudi Yusuph, alidai mnamo Februari 5, mwaka huu eneo la Mbweni, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa aliiba simu mbili aina ya Samsung na Itel yenye thamani ya Sh 350,000, begi moja la mkononi na fedha taslim Sh 2000 mali ya Godberth Rujaju. Kabla na baada ya kuiba alimtishia kwa panga ili kuijipatia mali hiyo.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na kurudishwa rumande kutokana na shtaka hilo kutokuwa na dhamana hadi kesi yake itakaposomwa tena Machi 20, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles