25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa wa moyo waongezeka JKCI

AVELINE   KITOMARY  DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amesema  kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa moyo.

Katika kuthibitisha hilo alisema  awali kwa siku moja  katika  kliniki  walikuwa wakihudumia wagonjwa 100 hadi 150 lakini sasa idadi hiyo imefikia wagonjwa 300 hadi 500.

Kutokana na hilo Prof. Janabi alisema wamelazimika kuongeza muda wa kutoa huduma kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa mbili usiku.

Akizungumza jana, Dar es Salaam alisema sababu kubwa ya magonjwa ya moyo kwa watu wa wazima hasa shinikizo la juu la damu na mfumo mbaya wa maisha.

“Tumepiga hatua kubwa sana katika matibabu lakini namba ya wagonjwa imekwenda juu sana,tuna vitanda 150 tuna vyumba 9 ilitulazimu kuongea na Serikali jinsi gani tunaweza kupata nafasi Rais alitupa sehemu ya Muhimbili na sisi tukaifanya kuwa wodi ya watoto.

Kutokana na ongezeko hilo, Profesa Janabi alishauri watu kuwa na desturi ya kupima afya kila mwaka.

“Wale wanaogundulika wakiandikiwa dawa na kufuata taratibu na kupima uzito, itasaidia madhara ya shikizo la damu yasifike kwenye moyo, vitu kama uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe vinatakiwa viepukwe na kutokufanya mazoezi ni tatizo hivyo uchaguzi ni mtu, ukiwa bize sana iko siku ugonjwa utatokea na utakuwa bize na wewe,”alibainisha Prof. Janabi.

Aidha kwa upande wa watoto alieleza kuwa sababu ya matatizo ya moyo ni mama kuwa na umri mdogo, mfumo mbaya wa ulaji kama matumizi ya vilevi na  kutokuhudhuria kliniki kunafanya watoto kupoteza maisha .

“Ukiwa mjamzito wiki 20 kwenda juu tunaweza kutambua mtoto atazaliwa na tundu moyoni  hivyo ukienda kwa daktari wako atakupa maelekezo ya mtoto kutozaliwa kwa njia ya kawaida au asijifungulie nyumbani aende hospitali kwani mtoto anaweza kupoteza maisha baada ya muda mchache,” alisema.

Pamoja na hayo Prof. Janabi alisema Serikali inaendelea kuboresha huduma za moyo nchini kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi.

“Mwaka jana tulifanya upasuaji wa kusimamisha moyo sasa Serikali imetuwezesha bilioni 4.6 za kununua mtambo wa kuwezesha operation hii itawezesha wagonjwa ambao mfumo wao wa umeme umeathirika.

“Kwasababu kuna aina mbili wale tunaowawekea ‘pace maker’  na wale ambao mioyo yao inakwenda mbio matibabu yake ni kuingia ndani ya moyo na kuchoma tuko katika hatua ya mwisho kabla ya mwisho wa mwaka tutatoa hiyo huduma,”alifafanua.

KUHUSU UPANDIKIZAJI MOYO 

Akizungumzia kuhusu huduma ya upandikizaji moyo alisema elimu inahitaji kwa kiasi kikubwa kutokana na ukubwa wa huduma hiyo.

“Jukumu kubwa ni kuelimisha wananchi kwanza  kupandikiza moyo  sio sawa na kupandkiza figo  kwani figo ziko mbili na moyo ni mmoja yule ambaye atatoa moyo maisha yake yataishia hapo na  ni nani sasa utampata hawa ni wale wagonjwa ambao wameshafikia hatua ya mwisho kabisa kwa nguvu za kibinadamu ,utaalamu,madaktari  chochote kile mtakachofanya huyu mgonjwa hata pona.

“Sasa hii inahitaji mgonjwa ambaye ataridhia atajitoa kwamba jamani mimi nikifikia hatua hii mchukue moyo wangu mumpe mtu mwingine ambaye utamsaidia tuna upima, halafu tunautoa na kumpa anayehitaji, sasa hivyo vitu jamii inatakiwa ielimishwe taratibu  sisi tutaongea na Wizara ya Afya  ikiridhia na kuomba kibali cha sheria kwasababu ni upandikizaji mkubwa,”alieleza .

Prof. Janabi alisema katika ujenzi wa jengo la kisasa linaloendelea kujengwa litawekwa miundombinu ya maabara ya upandikizaji moyo. 

 “Kwa pamoja kati ya China na Tanzania   walitoa bilioni 16 na sisi bilioni 10 kwa ajili ya kununua vifaa  tutaendelea kujenga,  hatua za kwanza zilishaanza lakini kutokana na matatizo ya wenzetu wa China waliyopata kidogo tumechelea mwanzoni walikuwa hapa na kundi la madaktari. 

Katika hatua nyingine Prof. Janabi amewashauri wananchi kukata bima ya afya ili kuweza kupata matibabu kwa urahisi zaidi na uwezo wa kupima afya mara kwa mara

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles