23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu Lesotho ashindwa kufika mahakamani kushtakiwa kwa mauaji ya mkewe

WAZIRI  Mkuu wa Lesotho,  Thomas Thabane (80), ambaye jana ilikuwa ashtakiwe kwa mauaji ya mkewe wa kwanza Lipolelo Thabane, hata hivyo alishindwa kufika mahakamani.

Mtoto wake wa kiume alilieleza Shirika la Habari la Reuters kwamba, baba yake alishindwa kufika mahakamani kutokana na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kuonana na daktari.

Awali polisi walisema walikuwa hawana uhakika juu ya mahali aliko.

Thabane ilikuwa awasili mahakamani saa tatu asubuhi lakini kufikia saa tano alikuwa hajafika.

“Bado najaribu kuthibitisha aliko au kama atafika au hatofika. hatujui,”  Naibu Kamishna wa Polisi Paseka Mokete alisema.

Thabane alitangaza kuwa atajiuzulu mwezi Julai kutokana na umri wake, bila kuzungumzia shutuma dhidi yake.

Mkewe wa sasa Maesaiah Thabane tayari ameshtakiwa kwa mauaji.

Atakuwa kiongozi wa kwanza kusini mwa Afrika kushtakiwa kwa mauaji akiwa madarakani, katika kesi ambayo imeishitua nchi hiyo.

Lipelo (58), alipigwa risasi na kufa siku mbili kabla Thabane kuwa Waziri Mkuu mwaka 2017.

Wakati huo, alieleza kuwa kitendo cha mauaji ya mkewe wa zamani ”hakina maana” lakini sasa polisi wanamshutumu kuhusika kwenye mauaji hayo.

Thabane alimuoa Maesaiah mwaka 2017

”Waziri mkuu atashtakiwa kwa mauaji”, Kaimu kamishna wa polisi Paseka Mokete alinukuliwa na shirika la habari la Uingereza, Reuters.

”Polisi wanaandaa miongozo na pengine atashtakiwa kesho,” aliongeza.

Thabane alisema kwenye redio ya taifa kuwa amelitumikia taifa kwa ”bidii” na kuwa atajiuzulu mwishoni mwa mwezi Julai, 

”Nimefanya kazi kwa ajili ya Lesotho. Leo…kwa umri huu, nimepoteza nguvu zangu nyingi,” alinukuliwa akisema.

MAUAJI YALIVYOTOKEA

Mkewe wa zamani, Lipoleo Thabane alipigwa risasi na kufariki nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Maseru siku mbili kabla ya kuapishwa kuwa waziri mkuu 2017.

Wanandoa hao walikuwa wakikabiliwa na mchakato wa kutalakiana.

Shambulio hilo lilidaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana , lakini stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani hivi karibuni na kamishana wa polisi , Holomo Molibeli zimezua maswali chungu nzima.

Agizo la kumkamata Maesaiah Thabane mwenye umri wa miaka 42 lilitolewa mwezi Januari baada ya kutoweka.

Alikamatwa katika eneo moja la mpakani na Afrika Kusini siku ya Jumanne baada ya makubaliano kati ya mawakili wake na maafisa wa polisi , alisema msemaji wa polisi Mpiti Mopeli akizungumza na chombo cha habari cha AFP.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles