WAFUNGWA MAELFU WATOROKA GEREZANI DRC

0
502
ULINZI: Polisi wakituliza ghasia wakati wakilinda gereza lililovamiwa mjini Beni, DRC.

 

 

KINSHASA,   DRC

WAFUNGWA zaidi ya 900 wametoroka baada ya watu wenye silaha kuvamia  gereza moja mjini  Beni, DRC.

Kwa mujibu wa Gavana wa Mkoa wa Kivu Kaskazini, Julien Paluku,  uvamizi huo uliotokea juzi na washambuliaji hao walitumia silaha kali.

Watu 11 wameripotiwa kuuawa katika tukio hilo na bado waliofanya mashambulio hayo hawajajulikana.

Shambulio hilo  ni la nne kwa wafungwa kutoroka jela kutokea nchini humo ndani ya   mwezi mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa polisi, wafungwa wapatao 4,000 walitoroka jela mwezi uliopita katika jela yenye ulinzi mkali katika mji mkuu wa Kinshasa ambako kundi la watu wanaopigania kujitenga lilihusishwa na hujuma hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here