KENYA YAZIMA MASHAMBULIO YA UGAIDI YA AL SHABAAB

0
704

 

 

NAIROBI,  Kenya

SERIKALI  ya Kenya imewakamata watu sita wanaotuhumiwa  wanamgambo wa kundi la al Shabaab walikuwa wamepanga kufanya mashambulio ya ugaidi.

Wiki za hivi karibuni, Kenya imepoteza takribani maofisa 20 katika mashumbulio ya ugaidi kwenye barabara iliyopo magharibi mwa nchi karibu na mpaka wa Somalia ambako wanamgambo hao walitumia vifaa vya milipuko.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Joseph Boinnet alisema katika taarifa yake kwamba washukiwa hao wawili ni raia wa Kenya na Somalia. Polisi   walikamata baadhi ya vifaa vya malipuko na kutengenezea mabomu.

Vikosi vya usalama vya Kenya vinashirikiana na vikosi vya usalama vya Somalia katika kuzima mashambulio na kukamata watuhumiwa.

Watu waliokamatwa wanahojiwa   kujua ukubwa wa mtandao wao, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Uingereza, Reuters.

Kenya imekuwa ikikabiliwa na changamoto za usalama mara kwa mara katika mpaka wake tangu ipeleke wanajeshi wake  Somalia mwishoni mwa 2011  kusaidia kupambana wapiganaji wa al Shabaab.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here