WAFUNGWA 17 WAUAWA WAKITOROKA DRC

0
492

KINSHASA, DRC

WAFUNGWA wapatao 17 wanasemekana kuuawa kwa kupigwa risasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mapema jana wakati wakijaribu kutoroka kutoka gereza kubwa lililoko mjini hapa.

Waziri wa Sheria, Alexis Thambwe Mwamba amesema wafungwa wapatao 100 wamekamatwa huku wengine 55 wakiendelea kusakwa, miongoni mwao akisemekana kuwa kiongozi wa kiroho wa waasi Ne Muanda Nsemi.

Inasemekana wafuasi wa kikundi chake cha Bundu Dia Kongo (BDK) wanadaiwa kushambulia gereza hilo la Makala alfajiri na kutorosha mamia ya wafungwa hao, kwa mujibu wa Mwamba.

Aidha miongoni mwa wafungwa wengine ni pamoja na aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha gerezani kwa mauaji ya rais wa zamani wa DRC, Laurent Kabila.

Maafisa wa usalama wameanzisha oparesheni kali mjini Kinshasa ili kuwakamata wafungwa hao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here