27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SAUDIA YAMWALIKA BASHIR KUKUTANA NA TRUMP

 

 

RIYADH, SAUDI ARABIA

SERIKALI ya Saudi Arabia imemwalika Rais Omar al-Bashiri wa Sudan, ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) katika mkutano wa kilele wa viongozi wa kiarabu na Kiislamu na Rais Donald Trump wa Marekani.

Ofisa aliyezungumza na Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) hakusema iwapo Rais Al-Bashir atakuwepo katika mkutano wa mwisho wa ngazi ya juu kabisa siku ya Jumapili.

Kuanzia Jumamosi, Rais Trump anatarajiwa kufanya ziara Saudi Arabia, ikiwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu alipoingia madarakani Januari mwaka huu.

Rais Bashir ameweza kukwepa kukamatwa tangu alipowekewa waranti na ICC mwaka 2009, kwa tuhuma za mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Jimbo la Darfur, ambako watu wasiopungua 300,000 wamepoteza maisha.

Haijulikani iwapo Bashir amekubali mwaliko huo.

Marekani si mwanachama wa ICC lakini imeunga muungaji mkono mkubwa wa kazi zake ikiwamo harakati za kutaka kumkamata Bashir.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles