23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Wafugaji, wakulima waibebesha mzigo Serikali

wafugajiNa Mauli Muyenjwa, Dar es Salaam
JAMII ya wakulima na wafugaji wamedai kutokumalizika kwa migogoro ya ardhi kati ya jamii hizo, inatokana na viongozi wa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wao.
Kauli hiyo ilitolewa na mwakilishi wa wakulima kutoka Wilaya ya Kilosa, Airu Mustafa katika kongamano la mwisho la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana.
Alisema suluhisho pekee la tatizo hilo, ni kutowapa nafasi watu wanaotaka uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
“Tulishapeleka malalamiko na kero zetu za migogoro isiyokwisha ili tukae meza moja, lakini hawajatatua matatizo hayo kwa kuwa wako kisiasa,” alisema.
Mwakilishi kutoka asasi ya kiraia ya Haki Jamii ya Garissa nchini Kenya, Abdi Sugara, alisema kutokuwapo asasi za haki zinazofanya kazi huru kunachangia haki kutopatikana.
“Watu hawajui wakimbilie wapi, Garissa ilikuwa imesahaulika, asasi yetu ambayo ni huru imefanikiwa kupambana na kuleta haki katika maeneo hayo ambayo yalikuwa yamesahaulika kwa kukosa huduma muhimu,” alisema Sugara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles