Wafanyakazi wa afya nchini msumbiji waomba ulinzi

0
656

-Msumbiji

Gavana wa jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji, Valige Tauabo amefanya mkutano na wahuduma afya katika mji wa Pemba kulikotokea mashambulizi ya kigaidi yaliyosababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa.

Gavana Tauabo alikutana na wataalamu wa afya kutoka miji ya Mocimboa da Praia, Macomia, Muidumbe, Quissanga na Palma waliokuwa wakifanya kazi kwenye vituo 40 vya afya ambavyo viliharibiwa wakati wa mashambulizi.

Pia katika mkutano huo walijadili namna ya kuendelea kuwasaidia watu walioachwa bila makazi huku wafanyakazi wa afya wakidai kuwa tayari kufanya kazi ikiwa watahakikishiwa usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here