22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Jimbo la New mexico kuruhusu matumizi ya Bangi

-Mexico

Gavana wa jimbo la New Mexico, Michelle Lujan Grisham Jumatatu alitia saini, muswada wa bangi uliopitishwa na bunge la jimbo hilo mwezi uliopita, na kufanya jimbo hilo kuwa la 17 kuidhinisha mihadarati hiyo kwa ajili ya matumizi ya starehe.

Ameyasema hayo Gavana Lujan Grisham ukurasa wake mtandao wa kijamii kuwa alichochea kupitishwa kwa sheria ya bangi mwezi uliopita, na kuweka sahihi yake ni katika kufuata taratibu.

“Kuhalalisha matumizi ya bangi kutabadilisha namna tunavyofikiri kwa mustakabali mzuri wa New Mexico, nguvu kazi yetu, uchumi wetu, kesho yetu”.

Wakati bunge la jimbo la New Mexico likipiga kura kuhalalisha bangi mwishoni mwa mwezi uliopita, walikuwa wakifanya hivyo saa kadhaa baada ya Gavana Andrew Cuomo kuweka saini kuhalalisha muswada wa bunge la jimbo la New York uliopitishwa usiku uliotangulia.

Kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi kwa watu wazima kulikopitishwa na majimbo hayo mawili katika kipindi cha saa 24 kunaonesha namna gani hatua hii inavyoendelea kukua kwa kasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles