22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Tunarudisha bando zote kama ilivyokuwa- TCRA

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema wanafuatilia kwa karibu sana na kwa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano nchini kuhakikisha kuwa suala la vifurushi vya simu linarejea kama ilivyokuwa hapo awali.

Akizunguza Dar es Salaam leo Jumatano Aprili 14, 2021, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Jabir Bakari amesema lengo ni kuona huduma hizo za vifurushi vya simu vinarudi kama ilivyokuwa hapo awali.

“Kama ambavyo maeleekezo ya serikali yanavyosema, tunafuatilia kwa karibu sana kuhakikisha kwamba mabando au vifurushi vinarudi katika hali yake ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali.

“Tunategemea siku siyo nyingi inaweza ikawa ni siku mbili au tatu tunafutailia karibu kila saa, maelekezo ni kwamba tunarudisha bando zote kama ilivyokuwa.

“Kilichotokea ni kwamba kampuni za simu zilikuwa zinatumia maelekezo mapya jambo ambalo limeleta changamoto, lakini sasa hivi tunarejesha huduma zote kama awali,” amesema Dk. Bakari.

Aidha, Dk. Bakari amesema kuwa sababu ya kubadilisha vifurushi hivyo awali ilikuwa ni kutokaa na kuwapo kwa wingi wa vifurushi hatua ambayo ilikuwa ikiwachanganya baadhi ya watuamiaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles