23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi TPC walalamikia kodi

sukariNa UPENDO MOSHA, MOSHI

CHAMA cha Wafanyakazi wa Huduma za Jamii Tanzania, (Tasiwu), tawi la Kiwanda cha Uzalishaji Sukari (TPC), kimemwomba Rais Dk. John Magufuli kupunguza makato ya kodi kwa mishahara ya wafanyakazi wa viwango vyote nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho katika tawi hilo, Bilal Mchomvu, wakati wa kusaini mikataba mipya miwili ya hali bora na mishahara ya wafanyakazi, wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

“Suala la Rais Dk. Magufuli kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi wengi, walilipigia makofi kumbe kulikuwa na kitu nyuma ya pazia.

“Nasema hivyo kwa sababu baada ya utekelezaji kuanza, sasa wafanyakazi wengi wameanza kushtuka, kwamba bado tunakatwa kodi na baadhi yetu hatujanufaika na punguzo hilo. Kwa hiyo, ni vema Serikali ikaangalia upya suala hili ili tusiendelee kuumia,” alisema Mchomvu.

“Katika suala hili la kodi, Serikali inasema kila mfanyakazi asiyekuwa na pato lisilozidi Sh 170,000 kwa mwezi, hakatwi kodi yoyote na mfanyakazi aliyezidi juu ya kiwango hicho hadi kufikia Sh 360,000 kwa mwezi, anatakiwa akatwe kodi kwa asilimia 11.

“Kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa, mtu atakayekuwa na pato la shilingi 360,000 hadi shilingi 540,000, atakatwa kodi kwa asilimia  20 na yule wa pato la shilingi 541,000 hadi 720,000, atakatwa asilimia 25 na  mwenye pato la 721,000 na kuendelea huyo atakatwa asilimia 30 ya kodi.

“Kwa msingi huo, tunaona ni kwa namna gani msamaha huo haujawanufaisha wafanyakazi wote kama inavyodhaniwa, ndiyo maana tunamwomba Rais Magufuli aliangalie upya suala hilo,” alisema Mchomvu.

Pamoja na Serikali kuwa na nia njema ya ukusanyaji wa mapato kwa wingi ili kuboresha shughuli za maendeleo, mwenyekiti huyo alisema ni  vema punguzo hilo la kodi likawagusa wafanyakazi wote tofauti  na ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa Mchomvu, hatua hiyo itasaidia kuboresha masilahi ya wafanyakazi nchini kwa kuwa wengi wao hukandamizwa na makato makubwa ya kodi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Utawala wa  TPC, Japhary Ally, alisema kwa sasa mahusiano kati ya wafanyakazi na kiwanda yako vizuri.

“Hali hii imesababishwa na uwepo wa ushirikiano baina ya vyama vya wafanyakazi kiwandani hapa na uongozi wa kiwanda tofauti na ilivyokuwa zamani.

“Kufuatia juhudi zinazofanywa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi hapa TPC, masilahi ya wafanyakazi yamekuwa yakiboreshwa kwa kuwapo kwa mikataba iliyosheheni masilahi bora, jambo ambalo limechangia uzalishaji kuwa wenye tija,” alisema Japhary.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles