25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Wafanyabiashara wa vileo wasomewa mashtaka upya

Kulwa Mzee -Dar es salaam

MKURUGENZI wa Kampuni ya Jaruma General Supplies Ltd, Lucas Mallya na wenzake watano, wamesomewa upya mashtaka 23 ya uhujumu uchumi ikiwamo kukwepa kodi ya vileo, kuisababishia Serikali hasara zaidi ya Sh bilioni 31.48 na kutakatisha fedha hizo.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka hayo jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Issaya.

Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliwataja washtakiwa kuwa ni Mallya, Happy Mwamugunda, Prochesi Shayo, Geofrey Urio, Mhasibu Tunsubilege Mateni na Mkaguzi wa hesabu, Nelson Kahangwa.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa wote wanadaiwa kati ya Januari 2015 na Januari 7, 2020 jijini Dar es Salaam kwa pamoja waliongoza genge la uhalifu kwa nia ya kupata faida.

Inadaiwa shtaka la pili hadi la saba yanamkabili Mallya ambaye anadaiwa Juni 3, 2019 Dar es Salaam alighushi kutengeneza stempu ya ushuru akionyesha imetengenezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati si kweli.

Anadaiwa alitoa nyaraka hiyo ya kughushi TRA akionyesha ni halali wakati akijua si kweli na katika shtaka lingine inadaiwa Januari 7 mwaka huu, Chang’ombe A Temeke, Dar ea Salaam alikutwa na rola 93 za stempu zenye thamani ya Sh 80,516,000 alizozichapisha bila kibali cha Kamishna wa Mapato.

Mshtakiwa Mallya anadaiwa kati ya Januari 2016 na Desemba 31, 2019 Dar es Salaam, kwa kutengeneza stempu hizo za kughushi, alisababisha hasara kwa Serikali ya Sh 15,241,075,169, akikwepa kodi kiasi hicho cha fedha na shtaka la saba anadaiwa kutakatisha kiasi hicho cha fedha huku akijua zinatokana na zao la kukweka kodi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles