27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Madaktari wapo tayari kufanya kazi popote -MAT

Aveline Kitomary -Dar es salaam

RAIS Wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Elisha Osati, amesema madaktari ambao wanatarajiwa kuajiriwa na Serikali wako tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalumu na MTANZANIA Dar es Salaam jana, mara baada ya Serikali kutangaza ajira hizo, Dk. Osati alisema tayari wameshazungumza na madaktari hao.

“Hao vijana mimi nimeshawasiliana nao,  hata ‘list’ yao mimi ninayo, kwahiyo tumeshakubaliana kwamba nafasi wakipewa waende na karibu asilimia 99 wameshakubali na wamesema watafanya kazi popote, hata maeneo ya vijijini,” alibainisha Dk. Osati.

Alisema kuwa kutokana na ajira hizo, wanataraji mabadiliko makubwa katika utoaji huduma kwani wananchi wengi  sasa watapata huduma kwa haraka.

 “Matarajio ni kwamba huduma sasa zinaendelea kuwa rafiki kwa jamii na tunategemea watakaoenda wanaenda kuongeza nguvu kubwa na kuondoa changamoto za upungufu wa watumishi wa afya. Hata huduma za afya zinaweza kuwa nzuri,” alisema Dk. Osati.

Aidha Dk. Osati aliishukuru Serikali kwa kuweza kutekeleza ahadi hiyo na pia aliomba utekelezaji wa ahadi zingine.

“Madaktari hawa msaada wao sio kwa janga la coroma tu, na magonjwa mengine, hili ni jambo ambalo sisi tunashukuru kwa sababu tulimwomba rais na tumeona kuwa ametekeleza ahadi hiyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles