28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

Wachumi waonya mgogoro wa Trump na Bunge

WASHINGTON, Marekani

WATAALAMU  wa uchumi nchini hapa, wameonya kwamba kuendelea kufungwa kwa serikali kunaweza kuathiri ajira za watu zaidi ya  500,000     mwezi  huu.

 Kwa mujibu wa watalaamu hao,    jambo hilo linaweza kuongeza  wastani wa kukosa ajira kuwa juu ya asilimia  4.0 endapo mgogoro katia ya Rais Trump na Bunge  hutatafutiwa ufumbuzi kabla ya Ijumaa wiki hii.

Mgogoro huo   ulianza Desemba 22 mwaka jana, baada ya Rais Donald Trump   kuliomba Bunge kumuidhinishia dola bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kati ya nchi hii na Mexico.

Juzi hali hiyo ilisababisha watumishi wa serikali  wapatao  800,000 kukosa mishahara yao.

Idara ya kazi ambayo haijaathiriwa na mgogoro huo, inadai imeshafanya utafiti kwa waajiri na kaya na imebaini kuwapo tatizo la ajira na ukosefu wa malipo ndani ya wiki iliyopita  pamoja na  Desemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa utafiti wa idara hiyo, katika kipindi cha  mwezi huu kuanzia Januari 6 hadi Januari 19 mwaka huu,   wafanyakazi wengi wa Serikali  wapatao 380,000 watakuwa wamepungua  wakati wengine watakuwa wanafanya kazi  bila malipo, labda kama serikali itafunguliwa wiki hii.

“Hivyo, ikiwa serikali  itaendelea kufungwa hadi Januari 19 mwaka huu,   wafanyakazi wa serikali hawatapokea mishahara kwa wakati katika wiki hii ya utafiti.

“Inamaanisha kwamba tunatarajia kupungua    malipo  kwa watumishi kuanzia  500,000 hadi 600,000, “alisema Omair Sharif, ambaye ni mwanauchumi mkuu nchini hapa anayefanya kazi katika Benki ya  Societe Generale,    New York.

Alisema   hali hiyo inaweza  kusababisha kushuka kwa ajira  kila mwezi ikiwa ni mara ya kwanza  tangu Septemba 2010 na hivyo kumaliza kipindi cha  miezi 99  mfululizo wa upatikanaji wa ajira.

Mtaalam huyo alisema   endapo Bunge litachukua hatua za haraka kuwalipa wafanyakazi kama ilivyokuwa Oktoba  2013 wakati serikali ilipofungwa,   tatizo hilo linaweza likatoweka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles