24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wachina mbaroni kwa kutoa rushwa

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

JESHI la Polisi mkoani Dodoma, linawashikilia raia watatu wa China kwa kosa la kutoa rushwa ya Sh milioni 1 kwa askari wa jeshi hilo baada ya kuwakamata wakiwa na mashine za kuchezea kamari zikiwa hazina vibali pamoja na kutosajiliwa. 

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge,  amewazawadia askari hao watano shilingi milioni moja na nusu kama zawadi kwao huku jeshi hilo likitoa shilingi 50,000 kwa kila mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda Muroto, aliwataja Wachina hao kuwa ni Chen Xiang (35), Chen Ji (21) na Lin Bibi (30).

Alisema jumla ya mashine za kamari 77 na watuhumiwa 12 wamekamatwa wakiwemo raia wa China ambao ndio wasambazaji wakuu ambapo kati yao wakati wanakamatwa walikuwa na mashine 62 wakiwa wamezificha baada ya kupata taarifa kwamba kuna msako.

Kamanda Muroto, alisema Wachina hao walitaka kutoa rushwa kwa polisi kiasi cha shilingi milioni moja ambazo polisi walizikataa na kuamua kuwafungulia mashtaka ya kutoa rushwa kwa askari polisi.

“Mfano huu wa askari wetu kukataa rushwa kutoka kwa Wachina ni ushahidi tosha kwamba polisi hatukubaliani na jambo hili na tunataka kuwathibitishia kwamba tutakuwa wakali kwa wale watakaoshawishi kutoa rushwa au kupokea rushwa.”

Awali, RC Mahenge, alipiga marufuku uchezeshwaji wa kamari katika nyumba yoyote katika Mkoa wa Dodoma.

Pia aliitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha waende mkoani humo ili wakazikague mashine hizo.

SELEMANI NA VIFAA VYA WIZI

Wakati huo huo, Kamanda Muroto, alisema Jeshi hilo linamshikilia Selemani Mathayo (46), mkazi wa Rau madukani mkoani Arusha, kwa tuhuma za kukutwa na mali za wizi ambazo ni mabegi 20 pamoja na vifaa mbalimbali vya kupandia milima.

Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa katika kituo cha mabasi cha Kizota jijini Dodoma akiwa na mali hizo.

“Vifaa hivyo vilihifadhiwa kwa mtu huyo baada ya kuibiwa na Mtana Ramadhan, mkazi wa Rau Madukani, ambaye ni mtoto wa Selemani Mathayo, mtuhumiwa naye amekamatwa huko Moshi na uchunguzi wa kina unafanyika,” alisema Kamanda Muroto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles