27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Rais Tshisekedi azua jambo, waziri mkuu agoma kujiuzulu

KINASHASA, DRC

LICHA ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupiga kura na kumchagua rais mpya katika uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 23, mwaka jana, bado nchi hiyo imeendelea kubakia bila Serikali ikiwa ni wiki nne sasa tangu Felix Tshisekedi, alipoapishwa kuliongoza taifa hilo.

Mawaziri mbalimbali wa Serikali iliyokuwepo wameanza kujiuzulu mmoja baada ya mwingine, huku hatima ya Serikali mpya ikiwa bado haijajulikana.

Duru za kisiasa zinasema kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshisekedi, ameshindwa kuunda Serikali kutokana na mgawanyiko unaoikumba jamii ya wanasiasa nchini humo.

Wakati huo huo Waziri Mkuu, Bruno Tshibala, bado hajajiuzulu wadhifa wake kama Waziri Mkuu wala kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa Serikali yake, licha ya kuwa aliombwa kufanya hivyo.

Kwa upande wa uundwaji wa Serikali, kazi kubwa iko mikononi mwa Rais mpya, Tshisekedi, kwa vile ni rais ambaye anatakiwa kuteua Waziri Mkuu kutoka kambi ya walio wengi bungeni.

Kwa mujibu wa sheria, chama au muungano wa vyama unaopata zaidi ya viti 250 ndio wenye sauti na ambao utakuwa na ushawishi wa kulidhibiti Bunge hilo la DRC kwa miaka mitano ijayo.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), vyama hivyo vimenyakuwa jumla ya viti 288 kati ya 429 bungeni, huku vyama vya upinzani vikiambulia viti 141 tu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles