WABUNIFU wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali, Kiki Zimba na Martin Kadinda wameungana kwa ajili ya kufanya onyesho la mavazi la kuiombea amani nchi ‘Fashion For Peace’ kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Onyesho hilo litafanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa King Solomon, Dar es Salaam kuanzia saa mbili usiku.
“Hekima, Umoja na Amani ndio ngao zetu, ni muhimu kwetu vijana kuhakikisha tunadumisha na kulinda amani yetu tuliyoirithi kutoka kwa mababu zetu,” alisema Mustafa Hassanali.
Naye Martin Kadinda kwa upande wake, alisema wameamua kufanya onyesho hilo la amani kwa ajili ya kuhamasisha amani kwakuwa bila amani hakuna kitakachofanyika.
Onyesho hilo limeandaliwa na kampuni ya 361 Degrees, kiingilio ni Sh 60,000 kwa VIP na Sh 25,000 kwa kawaida.