Hemedi: Sifikirii kurekodi video nje ya nchi

0
1470

hemedi_suleiman_06NA THERESIA GASPER

MSANII wa muziki wa kizazi kipya na filamu za kibongo nchini, Hemedi Suleiman ‘PHD’, amesema hajawahi kufikiria kufanya video za nyimbo zake nje ya nchi kama wafanyavyo baadhi ya wasanii wenye kipato cha juu.

Hemedi, ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Memories’, alisema anachofikiria ni kushirikiana na wasanii kutoka nje na si kufanya video nje ya nchi wakati nchini kuna mazingira ya kutosha kunogesha video zake.

“Kitu ambacho kipo kichwani mwangu kwa sasa ni kufikiria kufanya kazi na wasanii wa nje, ili niweze kuupaisha muziki wangu kimataifa zaidi na kuweza kuitangaza vyema Tanzania, sifikirii video za nje,” alisema.

Hemed anatarajia kuachia video yake mpya ya ‘Memories’ alioufanyia katika mazingira ya nchini chini ya usimamizi wa studio ya Downvilla records.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here