26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Waasi 21 wa kundi la CODECO wauawa DRC

KINSHASA, DRC

WAASI 21 wameuawa katika kipindi cha siku tatu za mapigano baina yao na jeshi la serikali katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Luteni Jenerali Philemon Yav amesema katika makabiliano na waasi hao, wanajeshi wawili waliuawa na wengine wanne wakajeruhiwa katika eneo la Walendu Tatsi, mashariki mwa mji mkuu wa mkoa wa Ituri, Bunia.

Aidha aliongeza kuwa, eneo hilo sasa lipo chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali baada ya makabiliano hayo yaliyoendelea hadi Jumapili, na kulazimisha idadi kubwa ya wakaazi kukimbilia usalama wao mwishoni mwa wiki.

Waasi wa CODECO wanajumuisha wapiganaji ambao wanadai kutetea haki za jamii ya wakulima Walendu katika eneo la Djugu.

Mapingano baina ya wakulima wa jamii ya Lendu na wafugaji wa kabila la Hema yalianza mwaka 1999 na kuendelea hadi 2003 katika mkoa wa Ituri wenye utajiri wa dhabau na mafuta ambapo makumi ya maelefu waliuawa.

Kundi hilo sasa limegawanyika kwa miezi kadhaa huku baadhi ya wanamgambo wakikatoa wito wa kuweka chini silaha.

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles