26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Libya yamtaka Macron awaombe radhi Waislamu duniani

TRIPOLI, LIBYA

WIZARA ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya imelaani matamshi ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na Uislamu na kumtaka afanye haraka kuwaomba radhi Waislamu duniani.

Mohamed al Qablawi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa habari wa “al Arabi 21” na kuongeza kuwa, matamshi yasiyo ya heshima ya rais wa Ufaransa yamezidisha chuki na hasira dhidi yake na bila ya shaka ametoa matamshi hayo ili kujinufaisha kisiasa katika chama chake.

Vile vile amekumbushia hukumu ya Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu iliyotolewa mwaka 2018 ambayo ilisisitiza kuwa, kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW si sehemu ya uhuru wa kujieleza na kumtaka Macron afute kauli zake za kichochezi na awaombe radhi haraka Waislamu kote ulimwenguni.

Kabla ya hapo pia Baraza Kuu la Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya ililitaka  shirika la mafuta la Marathon la nchi hiyo livunje mkataba wake na shirika la mafuta la Total la Ufaransa, kama sehemu ya kuonesha hasira za Waislamu kwa matamshi ya kifidhuli ya rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron.

Mbali na kuwatukana Waislamu, hivi karibuni Macron alitoa matamshi ya kifidhuli na kijuba dhidi ya Uislamu na Bwana Mtume Muhammad SAW akijigamba kwamba Ufaransa itaendelea kusambaza vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume huyo mtukufu. Ikumbukwe kuwa Waislamu wanaunda takriban asilimia 10 ya wananchi wa Ufaransa.

AP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles