Waziri mkuu atetea uamuzi wa utoaji mimba

0
283

WARSAW, POLAND

WAZIRI Mkuu wa Poland ametetea uamuzi wa mahakama kuhusu utoaji mimba, uliozua utata mkubwa na ambao umesababisha maandamano ya hasira kote nchini humo , yakitaka kukomesha kile wanachokiita ushenzi. 

Maandamano yamefanyika Poland kwa siku sita mfululizo kupinga hukumu hiyo, ambayo itaharamisha utoaji mimba isipokuwa katika mazingira ya kwenye ubakaji, na wakati maisha ya mama yako hatarini. 

Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki aliwaambia waandishi habari kwamba vitendo vya ushari, ushenzi na kuharibu mali havikubaliki kabisaa, na kuonya kwamba maandamano yoyote ya vurugu yanaweza kusababisha uchochezi. 

Poland ambayo ni nchi yenye waumini wengi wa Kikatoliki, tayari ina baadhi ya sheria kali zaidi ya utoaji mimba barani Ulaya na wanawake wengi husafiri nje ya nchi kutoa mimba. 

Lakini mahakama ya katiba ulitoa hukumu wiki iliyopita, ikiunga mkono sheria kali zaidi, na kubainisha kwamba sheria iliyopo sasa ambayo inaruhusu utoaji mimba pale ikigundulika mtoto aliyeko tumboni ana kasoro haikuwa inaambatana na matakwa ya kikatiba.

AP

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here