26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

‘WAAFRIKA HAWAFUNDISHWI MAPAMBANO DHIDI YA UNYONYAJI RASILIMALI’

Na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama amesema watoto wengi Afrika hawafundishwi mapambano ya pili dhidi ya unyonywaji wa rasilimali za bara hilo.

Amesema hayo leo Jumatano Aprili 11, katika kongamano la miaka 10 ya Kigoda cha Mwalimu linaloendela katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema pamoja na wadeni wengi kunyonya rasilimali hizo pia hata baadhi ya Waafrika wenyewe wamekuwa wakishiriki kutorosha rasilimali hali iliyosababisha wananchi wengi kuendelea kuishi katika umaskini mkubwa.

“Hivi karibuni tumeshuhudia benki ya dunia ikizitaja baadhi ya nchi za Afrika ikiwamo Tanzania na Ethiopia kufanya vizuri katika ukuaji wa uchumi huku mataifa ya Afrika yakionesha kuongezeka kwa pato la mataifa hayo (GDP).

“Wengi wetu hapa tulifundishwa shuleni namna ambavyo jitihada za kupinga unyonywaji wa rasilimali zetu kupitia makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa kule katika mkutano wa Berlin, lakini sasa watoto wetu hawafundishwi mambo haya,” amesema Profesa Penina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles