22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

MASHABIKI WAMLIZA SALMAN KHAN

MUMBAI, INDIA


Mashabiki mjini Mumbai nchini India, mapema wiki hii walimliza staa wa filamu, Salman Khan, baada ya kujitokeza kwa wingi kumpokea mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.

Staa huyo wiki iliyopita alihukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kuua aina ya swala ambao ni adimu sana nchini humo. Tukio hilo alilifanya mwaka 1998.

Khan alihukumiwa na kuwekwa ndani siku mbili katika gereza la Jodhpur Central lililopo mjini Jodhpur, hivyo wiki hii alikwenda mjini Mumbai kwenye makazi yake na kupokelewa na idadi kubwa ya mashabiki.

“Nawashukuru sana kwa mapokezi yenu, sikutegemea kama watu wangejitokeza kwa wingi kuja kuniona, furaha nilionayo nashindwa kuielezea, nimejikuta nikitokwa na machozi kwa furaha hasa baada ya kuwaona kwa wingi, nawashukuru sana na Mungu awabariki,” aliandika msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles