23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

PREZZO, JAGUAR WAMALIZA TOFAUTI ZAO

NAIROBI, KENYA


RAPA Jackson Makini maarufu kwa jina la Prezzo, amethibitisha kumaliza tofauti na staa mwenzake, Charles Kanyi, baada ya kuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu.

Mastaa hao wakubwa nchini Kenya wamekuwa wakirushiana maneno mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari, lakini sasa hali hiyo imefikia mwisho.

“Naomba niweka wazi kuwa, sina tatizo na mtu yeyote kwa sasa, wapo ambao nilikuwa nimetofautiana kutokana na baadhi ya mambo, ila kwa sasa sina tatizo nao,” alisema Prezzo.

Prezzo aliwahi kusema hamjui mtu yeyote anayeitwa Jaguar, ila analijua aina ya gari inayoitwa Jaguar ambalo ni la kisasa kutoka nchini Uingereza na Jaguar mwingine ambaye alikuwa anamjua msanii huyo ni mnyama na si binadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles