25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Vyama 13 vyataka mazungumzo yaendelee miswada sheria za uchaguzi

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Vyama 13 vya siasa visivyo na uwakilishi bungeni vimesema bado kuna nafasi ya kuendelea kuzungumza na kufikia muafaka kuhusu miswada ya sheria za uchaguzi na mswada wa sheria ya vyama vya siasa badala ya kutumia njia zinazoweza kuhataraisha amani.

Miswada hiyo ilisomwa bungeni kwa mara ya kwanza Novemba 2023 na hivi sasa wadau mbalimbali wanaendelea kutoa maoni kwa lengo la kuiboresha.

Akizungumza Januari 17,2024 na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Democratic Part (DP), Abdul Mluya amesema dhamira yao ni kulinda amani na utulivu uliopo nchini na kushauri viongozi wa vyama vya siasa watumie njia sahihi ili kufikia mabadiliko.

Katibu Mkuu wa Alliance Democratic Part (ADC), Doyo Hassan, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam.

“Viongozi wa vyama tuache kupinga kila jambo na tuache kuhamasisha fujo, tukae mezani…maandamano ni njia ya mwisho kabisa, tuiamini Serikali na Bunge ili kuendelea kuboresha muswada uliopo,” amesema Mluya.

Naye Katibu Mkuu wa Alliance Democratic Part (ADC), Doyo Hassan, amesema Rais Samia anapaswa kupongezwa kwa sababu amewarudisha Watanzania katika hali ya kujadiliana hivyo akashauri busara iendelee kutumika kuepusha taifa kuingia kwenye machafuko.

Katibu Mkuu wa Democratic Part (DP), Abdul Mluya, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa United Democratic Part (UDP), Swaumu Rashid, amesema miswada hiyo itawezesha kutungwa kwa sheria zitakazosaidia kurudisha uwajibikaji ndani ya vyama vya siasa na kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi.

“Tunataka wanawake wenye sifa na uwezo, tukiongeza uwajibikaji ndani ya vyama vyetu tutatengeneza wanawake wenye uwezo,” amesema Swaumu.

Hivi karibuni wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa kujadili miswada hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenister Mhagama, aliwahakikishia wadau wa demokrasia kuwa Serikali itazingatia maoni yote yatakayotolewa na kusisitiza kuwa hakuna kitakachochakachuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles