23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

Kamishna TAWA ampongeza Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Nyanda, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha taasisi hiyo kukamilisha mradi wa jengo la ofisi lenye thamani ya sh milioni 250.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo iliyofanyika jana Januari 16, 2024, Makao Makuu ya Ofisi za Pori la Akiba Moyowosi zilizopo Kifura wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mabula amesema jengo hilo lina jumla ya vyumba nane.

“Tunamshukuru Dk. Samia amefanya kazi nzuri ya kutupatia fedha zilizotuwezesha kukamilisha mradi huu na miradi mingine tunayoitekeleza ikiwa ni pamoja na mishahara, yote hii ni matokeo ya Serikali yetu, ndiyo inayotuwezesha,” amesema Kamishna Mabula.

Aidha amewataka wahifadhi wa Pori la Akiba Moyowosi kuhakikisha wanalitunza vizuri jengo hilo ikiwa na pamoja na kuimarisha usimamizi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na TAWA ndani ya hifadhi hiyo.

Katika hatua nyingine, Kamishna huyo ameupongeza uongozi wa pori hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kulinda rasilimali walizopewa kusimamia kiasi cha kuwavutia wawekezaji.

“Nimefarijika sana wakati napokea taarifa yenu kujulishwa kwamba Pori la Akiba Moyowosi lina vitalu vya uwindaji wa kitalii sita na vitani kati ya hivyo vina wawekezaji.

“Niseme tu kwamba hawa wawekezaji hawajaja bure wamekuja hapa kwa sababu kuna rasilimali na hii rasilimali ipo kwa sababu ya kazi yenu nzuri, mmefanya kazi nzuri ya kuhakikisha wanyama walioko kule porini na mazingira yao yako salama kwa hiyo niwapongeze sana kwa hilo,” ameongeza.

Kwa upande wake Kamanda wa Pori la Akiba Moyowosi, David Mnyapwani, ameipongeza Serikali kupitia menejimenti ya TAWA kwa jitihada za dhati za kuwezesha miradi inayotekelezwa katika hifadhi hiyo kujengwa na kukamilika kwa wakati.

Ujenzi wa mradi huo ulianza kutekelezwa Mei 5, 2023 na kukamilika Septemba 9, 2023 na tayari umeanza kutumika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles