23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

VisionFund, yawafutia deni wafanyabiashara waathirika wa maporomoko Hanang

Na Esther Mnyika, Hanang

Taasisi ya kifedha VisionFund Tanzania kwa kushirikiana na Metro Life Assurance, wamewafutia deni la mkopo wa sh. milioni 22 wafanyabiashara sita wadogo na kati ambao ni waathirika wa maporoko ya udongo ya Mlima Hanang.

Wafanyabiashara wengine watano wamesamehewa marejesho ya miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi, 2024.

Akizungumza leo Januari 17,2024 mkoani Manyara alipokutana na waathirika hao na kukabidhi hundi hiyo ya msamaha kwa wafanyabiashara hao, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja, amesema athari za maporoko hayo yamegusa watu mbalimbali.

Amasema VisionFund Tanzania kwa kushirikiana na Metro Life Assurance waendelee kuboresha ushirikiano na Serikali na jamii katika mambo mbalimbali wakati wa shida na raha.

“Jumla ya wafanyabiashara 11 wamapeta athari katika biashara zao ambao sita wamewafutia mikopo kabisa, hawatalipa na watano wamesahemewa marejesho miezi mitatu wataaanza kulipa marejesho rasmii mwezi Aprili mwaka huu,”amesema Mayanja.

Amesema kwa kufanya hayo wametambua uhalisia wa taasisi yao kwa kujali wateja wao katika kipindi hiki kigumu kwa kutoa msaada wa haraka ambao ni muhimu kwa wafanyabiashara hao.

Aidha ametoa rai kwa taasisi zingine za kifedha kuonesha uhalisia na tabia ya taasisi jinsi ilivyo kwa wateja wao wanapopatwa na magumu na wanawasaidia vipi katika kipindi hicho.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kifedha VisionFund, Chilala Hakoom amesema lengo kubwa la taasisi hiyo ni kusaidia jamii na kuboresha ya mtoto kwa kuwezesha familia kupitia huduma za kifedha.

Amesema taasisi hiyo inatambua ugumu wa kifedha unaotokana na waathirika hivyo imechukua hatua muhimu kufuta mkopo kwa wadeni walioathirika kupitia huduma yao ya Bancassurance.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Metro Life Assurance, Amani Boma amesema wao kama bima wanajukumu la kushiriki katika jambo hilo kwa sababu wanahusika na majanga.

“Ni wajibu wetu kuungana na kushirikiana serikali katika masuala ya majanga na bima kushiriki kwa wakati na watanzania mnapaswa kuwa na bima ziwasaidia wakati wa matatizo,”amesema Boma.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa Katesh, Fura Massawe ambaye ni muathirika wa maporoko hayo amesema anawashukuru VisionFund kwa kutambua changamoto zinazowakabili kwa sasa ikiwemo kupoteza mali zilizosombwa na maji hivyo, wanaanza upya biashara.

Maporomoko ya udongo na mawe kutoka eneo la mlima Hanang yaliyokea Desemba 3, 2023 na kusababisha vifo vya watu 89 na kuacha zaidi ya 600 bila makazi hususan kwenye Kata za Gendabih,Ganana na Katesh.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles