23.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Emma Music waachia ‘From The Ground Up’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Bendi inayofanya vizuri muziki wa Injili kutoka Australia, Emma Music (Emma Musik), wamefungua mwaka 2024 kwa kishindo na albamu mpya FROM THE GROUND UP.

Happy Mbemba ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema ndani ya Emma Music kuna waimbaji na wanamuziki wenye asili ya mataifa mbalimbali sio Kongo pekee jambo linalofanya muziki wao uwe na ladha tamu.

Akizungumzia albamu ya FROM THE GROUND UP, Happy amesema ina jumla ya nyimbo saba na kwasasa inapatikana kwenye mitandao yote inayouza na kusikiliza muziki.

“Lengo ni kumtangaza Kristo kupitia vipawa ambavyo Mungu ametupa, albamu ya FROM THE GROUND UP ina nyimbo zenye mguso wa pekee kama vile My Worship, Wastahili, Satisfied tuliyomshirikisha Azoa, Motema, From The Ground Up, Simbanga na Emmanuel,” amesema Happy.

Aliongeza kuwa kwasasa mashabiki wanaweza kuipata albamu hiyo kwenye mitandao mbalimbali hasa YouTube kwenye chaneli ya Emma Music au kwenye link hii https://www.youtube.com/playlist?list=PLFSqvRy_hO9hGPspyGBdUBMEN–qCyQh0

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles