29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

VODACOM YAONGEZA MUDA UUZAJI HISA ZAKE

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, imetangaza kuongeza muda wa uuzaji wa hisa zake hadi Mei 11.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia, alisema hatua hiyo inatokana na kupokea maombi mengi ya kutaka kununua hisa za kampuni hiyo.

“Vodacom Tanzania PLC inatarajia kupokea maombi mengi ya kununua hisa katika kipindi cha wiki hii.

“Pia kutokana na ushauri kutoka serikalini na makundi mbalimbali muhimu ya kijamii yanayohitaji kuwekeza, wakiwamo wabunge, makundi ya watumishi wa kada mbalimbali wa serikali na maofisa wa vyama vya ushirika kutoka sehemu mbalimbali za nchi, tumewasilisha maombi na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya Mei 11, mwaka huu,” alisema Mworia.

Mkurugenzi huyo alisema kuongezeka kwa muda wa mwisho wa kununua hisa kutawezesha wanaohitaji kununua hisa kwa makundi binafsi na taasisi zilizoomba muda uongezwe kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.

Alisema wanatoa shukrani kwa Watanzania ambao wamejitokeza kuwekeza kupitia kununua hisa na kuwakaribisha ambao bado hawajanunua kuchangamkia fursa hiyo katika muda huo wa nyongeza.

“Mgawanyo na mchanganuo wa umiliki wa hisa inapendekezwa utafanyika kuanzia Mei 19, mwaka huu na kuendelea kabla ya kumaliza mchakato wa mwisho wa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam katika tarehe iliyopangwa ya Juni 6, mwaka huu,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles