29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

MAREKANI: KOREA KASKAZINI ILIKUSUDIA KUFANYA UCHOKOZI

Marekani imesema Korea Kaskazini ilikuwa na nia fulani ilipotekeleza jaribio la kombora ambalo lilifeli mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Ulinzi James Mattis amesema jaribio hilo lilikuwa la kutojali na kwamba Marekani inafanya kazi kwa karibu na China kukabiliana na Korea Kaskazini.

Amesema Korea Kaskazini ilifanya hivyo ikikusudia kufanya uchokozi fulani.

Marekani ilisema kombora hilo la Korea Kaskazini lilipuka muda mfupi baada ya kurushwa angani.

Pyongyang imesema inaweza kuwa ikifanyia majaribio makombora kila wiki na pia ikaonya kwamba kutatokea "vita kamili" iwapo Marekani itaichukulia hatua za kijeshi.

"Iwapo Marekani wanapanga kutushambulia, tutajibu kwa shambulio la nyuklia kwa mtindo na njia yetu wenyewe," alisisitiza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Han Song-ryol

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles